Friday, April 25, 2014

Madrid waanza vema nusu fainali, wailaza Bayern 1-0.

Timu ya soka ya Real Madrid ya Hispania jana iliibuka mshindi katika mechi ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
madrid-waanza-vema-nusu-fainali-wailaza-bayer
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu, ilikua na ushindani  wa aina yake. Goli peke katika mechi hiyo lilifungwa mnamo dakika ya 19 na Mfaransa, Karim Benzema baada ya kuunganisha pasi safi kutoka kwa Modric.
Mechin ya marudiano itachezwa Alianz Arena huko Ujerumani, wiki ijayo.
Endapo Madrid watafanikiwa kuingia fainali wataandika historia nyingine kwani ni zaidi ya miaka 12 sasa hawajaingia katika fainali hizo.

No comments:

Post a Comment